Dubara (sehemu ya kwanza)
Karibu sana ndugu msomaji , hutojutia kupoteza Mb zako kwa hadithi hii iliyotungwa kwa mikasa , akili na ubunifu wa hali ya juu.
Umewahi kusikia mikasa za kutisha? Hapana hii INA mikasa ya kutisha na kinyama zaidi ya hio uliyopata kusikia.
Umewahi kusikia viumbe wa ajabu? Hapana hapa utaona na kujua viumbe wa ajabu.
Utakaposoma mpaka mwisho utastaajabu mno , Ow my god nashindwa hata jinsi ya kukwambia.
SEHEMU YA KWANZA:
DUBALA
Tangazo; marufuku kujimilikisha kazi hii kwa kuchapisha kwa jina lako na kuuza bila lidhaa.
Utakaposoma mkasa huu mwambie na mwenzako asome mkasa huu.
~ Ulikua muda wa usiku, ninaposema usiku basi ni usiku wenye giza nene. Ni ndani ya msitu mzito (bado hatujaujua unaitwaje)
Msitu huo ni wa ajabu sana tena sana , hapo mwanzoni 1905 walikuwako watalii ambao huenda kutalii bila shida , lakini msitu huo ukawa wa ajabu na wakikatili kupita misitu mwingine duniani , watu waliokuwa wakienda huko basi hawakufanikiwa kurudi, na watu hawakufanikiwa kujua kuna nini kwa sababu kila mwenye tamaa ya kujua , atakapoenda tu harudi kamwe. Sijajua wanakufa , ama wanapotea ama ni kuzuuuuriii kiasi kwamba hawataki kurudi nyumbani tena.
Msitu huo ulibakiwa na wanyama wakali wala nyama na wakaanza kuwindana wao kwa wao kimakundi. Na inasemekana endapo hawataacha kuwindana kimakundi , basi yatabaki makundi machache sana , itafikia mpaka mnyama jike kubeba mimba na atakapozaa atakula watoto wake mwenyewe.
Kikundi cha wanasayansi pamoja na serikali , walikaa pamoja na kujadili kwanini wachunguzi hawafanikiwi kurudi? Kama vile mchunguzi mkubwa nchini (bado haijatajwa nchi gan) bwana Robert Steven , zaina peter na wengine kibao takribani watu 13 hivi hawakufanikiwa kurudi , mbali na watu binafsi (kwa sensa imesemekana RAIA 34 hivi hawajulikani walipokwenda wala miili yao.
Dr John Silverton alipata nusu ufumbuzi wenye fumbo na maswal kibao.
Doctor huyu J.SL alituma kamera angani (je iliona nini?)
Camera hii iliwapa majibu nusunusu kwa sababu kamera hio ilizima baada ya kufanikiwa kupata picha moja.
Waliona mdudu wa kutisha, lakini alikua kama mtu , ila huenda ilikua mti tu kwa sababu ya uoga wao wakasema mtu , lakiniii hata kama ilikua ni mti kwanini mti huo umefunikwa na kipande cha nguo wenye uziuzi kama wa dunia ya kawaida?
Sawa tuseme labda ni mti umefunikwa na kipande cha kitambaa ,je mwenye kipande cha nguo hicho alipatwa na nini?
Hata ingekua ni wewe usingepata jibu kamili . aliuawa na nini maswali ni kibao.
Doctor huyo alipeleka picha hio serikalini. Hawakuamini walichokiona pia wakaomba kushirikiana nae. Hakukataa wala kusumbua aliwapa ushirikiano moja kwa moja kwa sababu alijua hili ni tatizo linalowakabili wao.
Huwezi amini kamera ya pili iliona mtu , mtu akitembea .............
Je wewe umeona nini?
Mi naona MTU huyo au? !
Endelea kuifatilia fizomedia.
Karibu sana sehemu ya pili.
https://www.mediafire.com/file/dghssu7mawhf612/Screenshot_20210113-081137.png/file
No comments