Dubara (sehemu ya pili)
Karibu katika sehemu ya pili ya mkasa mzito uliopewa na kutambulika kwa jina Dubala.
Endapo hujaipata sehemu ya kwanza nenda sehemu ya chini kabisa ya kutafuta andika, Dubala utaipata kirahisi sana. Ahsante.
DUBALA SEHEMU YA PILI;
Basi tukiacha ule uchunguzi wa mtaaramu doctor Steven pamoja na kamati ya wanasayansi wa kiserikali ipo hivi....
Kuna kijana anayeitwa John Steve , kijana huyu alikua na miaka 19 mwaka huo wa kizaa zaa wa 1909.
Kijana john alikua katika safari na mama yake kutoka kijijini kwao, kwenda kusoma shule ya upili mabondeni hills sekondari.
walipokua kwenye gari ilikua majira ya saa 11 hivi jioni karibu na msitu huo wa kutisha walikutana na kundi la watu wakutisha kama saba hivi, wakalisimamisha gari watu hao walihitaji mtu mmoja wa kumtoa kafara katika msitu huo, wakidai kuwa mungu wao anahitaji kafara ya hadharani.
Basi waliambiwa wamchague mmoja kati yao , walikua wakibabaika na kushindwa kabisa wa kumtoa kafara hio.
Ili kuonyesha wanachosema ni kweli wanamaanisha ni kweli basi wao walimuua MTU wao mmoja mbele yao kikatili sana. Hapo ndipo walipojua kuwa watu hawa ni makatili sana. Kisha mmoja akautoa moyo na kuutafuna mbichi. machozi yaliwamiminika wakijua bado zamu yao.
Basi kundi hilo la makatili waliamua kuondoka bila kuwafanya chochote na kuondoka , Hofu kubwa majonzi na kustaajabu ukatili huo , waliamua kuondoka haraka-haraka ili kuuvuka msitu huo. Basi walifanikisha kufika umbali flani hivi kama mita mia moja tu na dereva kwa sababu ya hofu alidondosha gari.
Gari hio ilidondoka bondeni kabisa ndani ya msitu huo, kibaya zaidi mama yake John alipoteza maisha palepale msituni (Msitu wa dubala)
ilimuuma sana kumpoteza mama yake. Basi alitoka ndani ya hilo gari lililodondoka na kuangua kilio kikubwa sana, aliumia sana moyoni. inachoma sana moyo ndugu yangu unachoma mno , mno.
Walipona watu wanne tu katika gari hio. Walitoka kwa kujilazimisha ndani ya gari kutoka nje sababu walikua wanamajeraha makubwa .
Basi baada ya kutoka kwenye ile gari walikaa pembeni kwa mda flani hivi, basi waliamua kuondoka eneo lile, lakini walipotaka kuondoka eneolile walishuhudia gari ikilipuka kabisa-kabisa. Walilia sana , lakini hakuna wa kuwafariji.
Sasa katika hao wanne waliokuwa salama , alikuepo baba mmoja, kijana anayejulikana kwa jina la Steve , mtoto lika la john alikua anaitwa lozy.
katika msitu huo huwezi kuona vizuri, kuna nyoka wa hatari sana na wanafanana na mimea kabisa. Ghafla yule baba alimezwa na nyoka huyo, walipoona tukio hilo walikimbiaa sana na hawajui wanapoelekea kabisa.
Walipofika sehemu flan walikuta kuna mti wenye matunda flan mazur lakini hawakujua yanaitwaje basi sababu ya njaa Walikula matunda hayo na mengine walibeba kwenye kifungashio sababu hawajui wanapokwenda.
Ghafla walisikia mtu anamwita john
Kwa sauti kubwa John john ilikua ni usiku sana wakaanza kukimbia ovyoovyo na kupoteana, ni usiku sana sana mtu huyo hakuacha alienderea kuita John john
Itaenderea ,
No comments