Jinsi ya kuishi na Mtu msomi

 Habari msomaji wetu wa fizomedia 

Leo tutazungumzia kiundani kumjua na jinsi ya kuishi na MTU msomi.


Watu wengi huwa tuna malengo ya kusoma sana kuwa MTU anayefahamu vitu vingi duniani kuwa mdadisi kiufupi , OK tusiende mbali sana , tuyajue malengo ya msomi kabla ya kuwa msomi na kupata kazi yake.


1. Hutamani kuja kuwa msaada mkubwa kwa watu.

Msomi yoyote hutamani kuja kuwa msaada kwa watu , kwanini nasema hivo?  Mfano hai huu apa MTU anayesomea udaktari huwa na moyo wa msaada kwa watu , anapoipata hio kazi hujitahidi kadri awezavyo juu chini mgonjwa apone. Endapo mgonjwa hatopona nafsi yake husononeka sana na kumpa maumivu makali mno. Kwa sababu kila msiba ukitokea msiba huo unamhusu yeye pia.


2. Hutamani Siku moja kuja kuwa MTU anayejulikana kwa kutoa misaada.

MTU huyu ni MTU anayetamani kupewa sifa ya kutoa msaada kwa watu wengi. 

Zipo sifa nyingi anazopenda na sifa hizo ni nzuri sana na ni malengo mazuri sana.

Je, umewahi kuuliza njia ukaambiwa ukifika mbere nyoosha na ukakuta njia hio imepinda? Ulifanyaje , huenda uliamua kuuliza MTU mwingine , sawa akakwambia ow mbona umepaacha? Rudi nyuma....

Malengo ya msomi hubadilika kadili yeye anavoruhusu mambo au fikra zimbadilishe.

1. Msomi huyu huwa hakubali kushindwa.

Ngoja nikupe mfano huenda yeye kasomea uchumi , lakini inapotokea mada tofauti na aliyosomea huwa anajitahidi kuunda hoja zake ili kuonekana anajua kitu hicho.

Ili uweze kuishi nae kubali kushindwa vitu vingine, sababu ni MTU anayeona anajua kila kitu ingawa hajui vingi.


2. Huwa na tabia ya kuweka matabaka.

Hupenda kuchagua marafiki wasomi wenzake, huwadharau watu wa hali ya chini na kushikamana na marafiki wapya.

Hivyo kama una rafiki anayesoma wewe husomei kitu chochote upo mtaani , usijiegemeshe sana  namaanisha usimtegemee sana MTU huyo atabadilika kama fikra zake ni nyepesi. Ishi naye kawaida tu usifanye kuwa yeye ni muhimu katika maisha yako, kwa sababu yeye pia ni MTU mwenye akili , wewe unaona yeye ni muhimu katika maisha yako lakini yeye anaona ni muhimu sana katika maisha yake yeye kuliko maisha yako wewe.

3. Hujiona ni bora kuliko wengine.

Hii inaereweka kabisa nadhani umewahi kujionea mtaani,  .......

........................



 Ewe mwanafunzi ewe mzazi,

Elimu ni kitu chenye faida kubwa sana hapa duniani , japo tunajua dunia si ya kudumu,  faida ziko nyingi sana kuliko hasara zake. 

Kwahiyo ni mimi Daniel Silvester, nilikua najaribu kukuonyesha ni jinsi gani unaweza kuishi na MTU aliyebadilika kifikra tofauti na ulivokua unamjua mwanzoni ?  Usipinge, watu hubadilika sana, huenda haijakutokea, basi waulize iliyowatokea. Au, Je, una marafiki wangapi wasomi wakubwa unaokaa nao na kupiga soga nao? 

Tafadhali kama wewe unasoma, usikate tamaa kabisa toa juhudi zako katika hilo, maana kuferi kimaisha huenda unahangaikia mambo mengi kwa wakati mmoja.

        


                                  ,Daniel Silvester 

..ahsanteni kwa kusoma nakala hii.

No comments

Powered by Blogger.